KILELE CHA WIKI YA JAI: WANANCHI WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU DODOMA
Posted on: August 31st, 2025
Tarehe 23 Julai 2025, Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) kwa kushirikiana na Jamiyatul-Akhlaaq Islaam (JAI) wamefanya tukio la kilele na maadhimisho ya Wiki ya JAI katika Uwanja wa Mavunde Complex, Dodoma.
Wananchi walijitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu, na shughuli hiyo inaendelea kwa lengo la kuokoa maisha ya wenye uhitaji hospitalini.
Aidha, kabla ya kilele hiki, JAI iliendesha kampeni na mazoezi ya uchangiaji wa damu katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama.