Kuwasili kwa mashine za Apheresis
Posted on: August 31st, 2022
Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeanza kupokea mashine za Apheresis,Mashine hizi ni teknolojia ya kisasa inayowezesha wachangia damu kuchangia aina fulani ya chembehai au sehemu ya majimaji ya damu tu. Faida za teknolojia hii ni kuongeza ubora wa mazao ya damu na hivyo ufanisi wa matokeo ya matibabu Kwa wagonjwa wanaoongezewa damu. Vilevile inawawezesha wachangia damu kuchangia mara nyingi zaidi ndani ya mwaka mmoja na hivyo kuongeza upatikanaji wa mazao ya damu