Mganga Mkuu wa Serikali afanya ziara katika Kituo cha Mpango wa Taifa wa Damu Salama – Kanda ya Ziwa
Posted on: October 15th, 2025Mganga Mkuu wa Serikali amefanya ziara katika kituo cha Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Kanda ya Ziwa kwa lengo la kukagua na kujionea hali ya utoaji huduma za damu salama katika eneo hilo.
Katika ziara hiyo, Mganga Mkuu ameagiza kuanzishwa kwa mfumo wa usajili wa wachangia damu (Donor Registration System) utakaomuwezesha mchangiaji damu kujisajili mwenyewe kwa urahisi na haraka zaidi.
Aidha, amewashukuru wachangia damu wote kwa moyo wao wa kujitolea kuokoa maisha ya wengine kupitia uchangiaji damu salama, huku akisisitiza kwa nguvu suala la kutokuuzwa kwa damu, akibainisha kuwa damu ni zawadi ya uhai na inapaswa kutolewa bila malipo.
Vilevile, ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na serikali katika kusaidia upatikanaji na utoaji wa huduma za damu salama nchini.
Katika hatua nyingine, Mganga Mkuu wa Serikali amekutana na watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama – Kanda ya Ziwa, ambapo amesikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutoa maelekezo ya namna ya kuboresha mazingira ya kazi na utoaji huduma kwa wananchi.
Pia amehimiza ushirikiano wa karibu kati ya ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) ili kuboresha zaidi huduma kwa wananchi.
Mwisho, amesisitiza umuhimu wa kutengeneza mifumo bora na endelevu itakayosaidia kurahisisha utendaji kazi na kuhakikisha huduma za damu salama zinapatikana kwa ufanisi katika maeneo