Uchangiaji damu wa Apheresis


Apheresis ni nini?  

Apheresis ni tekenolojia ya  kuchangia aina moja au zaidi ya mazao ya damu kutoka kwa mchangia damu. Mazao haya ni kama : Chembe sahani (Platelets), chembechembe nyekundu za damu  (RBCs) na Plasma. Teknolojia hii huturuhusu kukusanya kile ambacho wagonjwa wetu wanahitaji na kurudisha damu iliyobaki kwa wachangia damu.      

Usalama wa wachangia damu ndio kipaumbele chetu. Mashine ya Apheresis huchakata damu ili kuitenganisha, huvuna mazao damu  yanayokusudiwa na kurejesha damu iliyobaki kwa mtu anayechangia damu.   

Je, apheresis ni salama kwangu?    

Ndiyo, uchangiaji kwa njia  ya apheresis ni salama sana. Kila mchangiaji anaangaliwa kwa karibu na wafanyakazi waliofunzwa ambao huhudumia wachangia damu wakati wote wa zoezi la uchangiaji.          

Je, kuna madhara yoyote wakati wa kuchangia damu kwa njia ya Apheresis?  

 Wengi wa wachangia damu kwa njia ya  apheresis hawapati madhara wakati wa zoezi la uchangiaji damu.. Wengine huhisi baridi kidogo au jambo ambalo si madhara makubwa na linaweza kudhibitiwa vyema na wataalamu waliofunzwa.    

Vigezo vya uchangiaji wa apheresis     

Vigezo vya uchangiaji kwa njia ya apheresis  ni sawa na uchangiaji  wa damu kwa niia ya kawaida. Mchaangia damu wa Apheresis lazima:   

• Awe na umri wa  miaka 18. hadi 65    

• Kuwa na afya njema. 

• Uzito usiopungua kilo 50. 

• Kwa mchangiaji wa chembe sahani kwa njia ya apheresis, jumla ya chembe sahani kwa mchangiaji  inapaswa kuwa zaidi ya 150 × 109/L.

 • Kwa mchangiaji wa plasma ya apheresis, jumla ya kiwango cha protini cha mtoaji kinapaswa kuwa zaidi ya 60 g/L. 

 • Kwa apheresis ya seli nyekundu mbili, mchangia damu wa jinsia yoyote wanahitaji kuwa na kiwango cha chini cha himoglobini cha 14.0 g/dl (68% HCT)