Maswali na majibu

KWA NINI UJITOLEE KUCHANGIA DAMU?

Hadi sasa hakuna utaalamu wa kuzalisha damu nje ya binadamu. Kwa hiyo, wewe ni miongoni mwa wanaopaswa kujitolea damu. Unapojitolea damu unashiriki kikamilifu kuokoa maisha ya binadamu

NI MARA NGAPI MTU ANATAKIWA KUCHANGIA DAMU KWA MWAKA?


  • Mwanamke anaweza kuchangia kila baada ya miezi minne.
  • Mwanamume anaweza kuchangia kila baada ya miezi mitatu

JE NAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI WAKATI WA KUCHANGIA DAMU?


Hapana.

Kuchangia damu ni kitendo salama kabisa kwani vifaa vyote vinavyotumikwa ni safi na salama hutumika mara moja kwa mtu mmoja.

JE DAMU YANGU ITAFANYIWA VIPIMO GANI?


Damu itapimwa vipimo vifuatavyo:-

  • Kiwango cha damu
  • UKIMWI (VVU)
  • Kaswende
  • Homa ya Ini (Hepatitis B na C)
  • Makundi ya damu.

JE NITAPEWA MAJIBU YA VIPIMO VYA DAMU YANGU?

Ndio

Utapewa majibu yako kupitia mshauri nasaha baada ya kupimwa. Vipimo vyote vya maabara hufanywa kwa usiri wa hali ya juu. Hakuna mtu yeyote atakayeambiwa majibu ya vipimo vyako bila ya idhini yako.

changia damu

changia damu

Je, huwezi kushiriki katika michezo au shughuli nyingine zinazohusisha kutumia nguvu baada ya kuchangia damu?

Kuchangia damu hakuathiri uwezo wa kufanya michezo, mazoezi au shughuli nyingine za mwili. Ushauri unaotolewa ni kuepuka kuinua vitu nzito au mazoezi magumu kwa siku nzima baada ya kutoa damu. Unaweza kuendelea na uinuaji wa vitu vizito au mazoezi magumu kwenye siku inayofuata hasa kwenye mkono uliochomwa sindano.

Je Vigezo/Sifa gani za mtu anayeweza kuchangia damu?

Mtu yeyote, mwanamke au mwanaume anaweza kuchangia damu kama ana vigezo vifuatavyo:

Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 65

Uzito usiopungua kilo 50

Kwa mwanamke asiwe mjamzito au anaenyonyesha

Asiwe na maradhi ya muda mrefu kama Shinikizo la damu, Kisukari, Kifafa, Pumu n.k

Awe mzima wa afya njema na asiwe na Homa

Asiwe na mienendo hatarishi ya kupata maambukizi ya magonjwa kama Homa ya Ini (B&C), UKIMWI (HIV/AIDS)

Mwanamke anaweza kuchangia kila baada ya Miezi 4 na Mwanaume kila baada ya Miezi 3.

Je, unaweza kupata maambukizi mbalimbali ikiwemo VVU wakati wa kuchangia damu?

Huwezi kupata maambukizi yoyote wakati wa kuchangia damu. Wafanyakaziwa Mpango ni watu wenye weledi na hutumia vifaa viliyotasishwa (sterile) na vikishatumika hutupwa kwa njia salama.

Why Should I Donate Blood?

Blood is needed to save lives in times of emergencies and to sustain the lives of those with medical conditions, like leukemia, as well as patients who are undergoing major surgeries. For many patients, blood donors are their lifeline. One unit of blood can save three lives, Blood and platelets cannot be manufactured; they can only come from volunteer donors.

Why Should I Donate Blood?

Blood is needed to save lives in times of emergencies and to sustain the lives of those with medical conditions, like leukemia, as well as patients who are undergoing major surgeries. For many patients, blood donors are their lifeline. One unit of blood can save three lives, Blood and platelets cannot be manufactured; they can only come from volunteer donors.