Mfumo wa usimamizi wa ubora

        

 Mpango wa Taifa wa Damu Salama unatekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora (Quality Management System) katika kazi zake zote kuanzia wakati wa kupata maeneo ya uchangiaji wa damu hadi huduma ya uangalizi wa mgonjwa baada ya kuongezewa damu salama katika vituo vya kutolea huduma za afya.       

Tathmini ya Umahiri wa Upimaji wa Damu katika Mabara      

 Mpango wa Taifa umejisajili na hushiriki katika mpango wa tathmini ya umahiri wa upimaji wa vipimo vya magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya damu na vipimo vya makundi ya damu. Tathmini hii inafanywa na shirika la Kimataifa kwa kufuata viwango vya ISO 17043 kwa ulinganifu na maabara nyingine zinazoshiriki tathmini hii kidunia.     

Vilevile Mpango wa Taifa wa Damu Salama una programu ya kuandaa sampuli na kuzisambaza kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kuvipima umahiri wake katika kufanya vipimo vya makundi ya damu kabla ya kuwaongezea wagonjwa damu (pre-transfusion testing). Mpango huandaa na kusambaza sampuli hizi chini ya mwamvuli wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Umma (NPHL).            

Pia Mpango wa Taifa wa Damu Salama una utaratibu wa kujihakikishia ubora wa mazao ya damu yanayozalishwa kwa kufanya uhakiki kwa kutumia vipimo vya maabara (Quality Control) na kufuatilia viashiria vya ubora wa mazao ya damu. 

Mafunzo      

Mpango wa Taifa wa Damu Salama umepanga utaratibu wa kujenga uwezo kwa watumishi wa kada za afya  kupitia mafunzo na ushauri kuhusu michakato ya kuhakikisha usalama wa damu, taratibu na mfumo wa usimamizi wa ubora.     

 Ulinganifu wa Vipimo    

Mpango waTaifa wa Damu Salama una akiba ya sampuli za damu zilizopimwa na kujulikana majibu yake. Sampuli zenye maambukizi ya magonjwa huhifadhiwa na hutumika kama sampuli za marejeleo kwa taasisi zinazohitaji kwa madhumuni ya udhibiti wa ubora ikiwa ni pamoja na uthibitishaji wa vipimo vya kimaabara (method verification/validation) na madhumuni mengine. Sampuli zinazotolewa zinaweza kuwa na alama nne za maambukizi ambayo ni VVU, Homa ya Ini B,. Homa ya Ini C & Kaswende) au serolojia ya makundi ya damu.    

NBTS produces and distributes Proficiency Testing (PT) materials for Blood Group Serology under the umberalla of the National Public Health Laboratory. The scheme implements ISO 17043 standard requirements for proficiency testing.