Nani anaweza kuchangia damu


Vigezo vya Kustahiki Kuchangia Damu      

 Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka  vigezo vya kuchangia damu. Madhumuni ya vigezo hivi ni kulinda usalama wa mchangiaji wa damu na mgonjwa. Maelezo ya vigezo hivi na vingine yanaweza kupatikana katika mwongozo ya uchaguzi wa wachangia damu wenye sifa (Donor Selection Guideline). Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:   

Umri: miaka 18-65    

Uzito: ≥50kg      

Kiwango cha hemoglobini: ≥12.5g/dl     

Hali ya kiafya: Mchangiaji damu anapaswa kuwa na afya njema, , asiwe na magonjwa kama vile kisukari, Shinikizo la juu la damu n.k, asiwe mgonjwa anayejulikana kuwa na VVU, Homa ya Ini B&C, Kaswende au maambukizi mengine yoyote yanayoweza kusambazwa njia ya damu kuongezewa damu.    

Muda wa kusubiri kabla ya kuchanga tena: Mchangia  damu anatakiwa awe ametoa awali kutoka miezi 3 au zaidi kwa wanaume na miezi 4 au zaidi kwa wanawake