sababu za kukuzuia usichangie damu


 Vigezo vya Kuahirisha    

Wachangia damu damu ambao hawakidhi vigezo vya kukubalika kwa ajili kuchangia damu huahirishwa kwa muda au kwa daima kulingana na sababu ya kuahirishwa.          

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo wachangiaji damu wanaweza kuahirishwa. Maelezo yanaweza kupatikana katika mwongozo wa uchaguzi wa wachangia damu wenye sifa (Donor selection guideline). 

 Umri: chini ya miaka 18 na> miaka 65 

 Uzito: <50kg    

Kiwango cha hemoglobini: <12.5g/dl  

Hali ya kiafya: Kutokuwa na afya njema, , kuwa na  magonjwa ya kudumu kama vile kisukari, Shinikizo la juu/chini la damu n.k, mgonjwa anayejulikana kuwa na VVU, Homa ya Ini B&C, Kaswende au maambukizi yoyote yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya damu.   

Muda wa kusubiri kabla ya kuchanga tena: Mchangiaji mtarajiwa wa damu alichanga ndani ya kipindi cha chini ya miezi 3 kwa wanaume na ndani ya kipindi kisichozidi miezi 4 kwa wanawake.    

Matibabu: Mchangia damu ambae amemeza aspirini au dawa kama hizo ndani ya saa 72 kabla ya kuchangia hawakubaliki kuchangia damu inayokusudiwa kutengenezwa zao la damu la chembe sahani  au kwa ajili ya platelet-pheresis.