Kukusanya damu
Mpango wa Taifa wa Damu Salama hukusanya damu kutoka kwa wachangiaji damu wa hiari (Voluntary-Non Remunerated Blood Donors).
Kuna aina kuu mbili za uchangiaji wa damu ambazo ni:-
1.Uchangiaji wa damu nzina (whole blood donation) na
2.Uchangiaji wa mazao mahsusi ya damu (apheresis donation) ambapo mtoaji damu hutoa sehemu maalum za damu tu kama:-
Chembe sahani (platelets),
Sehemu ya majimaji ya damu (plasma) au
Seli nyekundu.(Red blood cells)