Usimamizi wa matumizi sahihi ya damu


Mashirikiano ya Kitaalam kati ya Vituo vya Kutolea Huduma za Afya na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (Clinical interface)

Mpango wa Taifa wa Damu Salama hutoa miongozo na elimu kupitia mawasiliano na wafanyakazi wa vituo vya kutolea huduma za afya ili kuwafahamisha na kuwaelimisha kuhusu upatikanaji wa damu na mazao ya damu ikiwa ni pamoja na matumizi  yanayofaa.       

Mpango wa Taifa wa Damu Salama husaidia vituo vya kutolea huduma za afya kwa kutengeneza miongozo ya kimatibabu kuhusu matumizi yafaayo ya damu na mazao ya damu, kuhamasisha utendaji bora zaidi wa uongezaji wa damu salama kwa mgonjwa, na kuendeleza elimu  kuhusu uongezaji wa damu salama kwa mgonjwa kwa wafanyakazi wa vituo vya kutolea huduma za afya. Vilevile Mpango Taifa wa Damu Salama huviwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kwaa kutengeneza au kupitisha miongozo ya kimatibabu ambayo inatoa taarifa kuhusu mazao ya  damu, usimamizi wake pamoja na aina ya huduma zinazopatikana katika vituo vya Mpango.