Kuhusu mpango


Mpango wa Taifa wa Damu Salama  (NBTS) -Tanzania ni Programu iliyoanzishwa mwaka 2004 chini ya Wizara ya Afya. Ilianzishwa kupitia Mkataba wa Ushirika kati ya Wizara ya Afya ya Tanzania na Serikali ya Marekeni kupitia Shirika la CDC kwa ufadhili wa mkakati wa PEPFAR kama nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya janga la VVU/UKIMWI. Hivi sasa Mpango unaendeshwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya. Shughuli za Mpango wa Taifa wa Damu Sakama zinafanywa kwa ushirikiano wa karibu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).      

Mpango huu una jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote za usalama wa damu nchini ambazo ni pamoja na upatikanaji wa wachangiaji damu wa hiari, ukusanyaji wa damu kutoka kwa wachangiaji wa damu wanaostahili, uhifadhi wa damu, utengenezaji wa mazao ya damu, upimaji wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia  ya damu (TTIs), upimaji kwa serolojia ya makundi ya damu na ugavi wa damu salama na mazao ya  damu kwenye vituo vya kutolea huduma za  afya. Mpango wa Taifa wa Damu Salama pia hutoa miongozo kuhusu matumizi sahihi na yafaayo ya damu na mazao ya damu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.