JAMII YA KHOJA SHIA YAKUSANYA CHUPA 1437 ZA DAMU KWA KUSHIRIKIANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA

Posted on: August 28th, 2022

Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri Imeomboleza kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) aliyeuawa kikatili huko mji wa Kerbala nchini Iraq na Jeshi la Yazid.

Ambapo umeunga mkono uchangiaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama , Kampeni ya Kuhamasisha Uchangiaji Damu.

Akizungumzia juu ya Imam Hussein Shabani Ally ameziomba taasisi na jumuiya nyingine kuiga mfano wa Jumuiya hiyo kwa kujitoa kuchangia damu ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji.

“Tunaamini katika Imam Hussein kiongozi aliyejitoa kuwapigania wanyonge tutaendelea kupinga uonevu wowote kwa kuhimiza amani na utulivu kwa waislamu wote,” amesema Ally.

Aliongeza kusema kuwa uchangiaji uliofanywa na taasisi hiyo umeonyesha ni kwa jinsi wanavyojitolea kusaidia watu wenye mahitaji ya damu bila kujali itikadi rangi na dini.