KAMPENI YA THUBUTU KUWA JASIRI

Posted on: November 13th, 2023

Mpango wa Taifa wa Damu Salama umezindua kampeni ya uhamasishaji wa wananchi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kampeni ya kitaifa ya ukusanyaji damu ya mwezi Disemba,  2023. Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeamua kuipa msukumo wa kipekee Kampeni hii kwa kuwa itafanyika mwisho wa mwaka ambapo vyuo na shule nyingi zinakua zimefungwa. Pia ni kipindi ambacho ajali nyingi hutokea, hivyo kuongeza mahitaji ya damu. Mpango umejipanga kuhamasisha wananchi katika sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na maeneo ya masoko, vituo vya mabasi, maeneo ya wazi na sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu. Kampeni hii itadumu kwa miezi mitatu, kuanzia Octoba hadi Disemba, 2023. Kauli mbiu ikiwa ni ‘Thubutu kuwa Jasiri’ Changia damu, Okoa maisha.