KIKAO NA WADAU WA MAENDELEO

Posted on: October 27th, 2022

Kutoka Dodoma 27/10/2022

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amekutana na wadau wa Maendeleo @koicatanzaniaoffice KOICA na @uniceftz wanaofadhili miradi ya ujenzi wa kituo cha damu salama kanda Ya kati Dodoma na ujenzi wa mradi wa kuboresha huduma za afya ya Mama na Mtoto.

Prof. Nagu amemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ambapo amesema ujio wa wadau hao unalenga katika kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa dodoma