KUTOKA UNIT 659 MPAKA UNIT 1336 ZA DAMU KISARAWE

Posted on: September 10th, 2022


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon @NikkWaPili amewapokea Wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali Nchini wakiongozwa na Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe waliofika Kisarawe kwa ajili ya Shughuli mbalimbali za utalii.

Mara baada ya shughuli za Utalii Wageni hao walichangia Damu ambapo DC Nikki wa Pili amesema Kisarawe kwa mwaka ilifanikiwa kukusanya unit 1,336 za damu ikiwa ni asilimia 190 kutoka malengo ya awali unit 659 na kupelekea uzazi salama bila kuwa na kifo hata kimoja kwa mwaka 2021.

Shughuli ya uchangiaji damu iliratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kisarawe kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu salama.