MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KUHUSU USIMIKWAJI WA MASHINE ZA APHERESIS

Posted on: September 27th, 2022

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika kuendelea   kuimarisha na kuboresha huduma za upatikanaji wa mazao ya damu kuendana na huduma za matibabu maalumu na bobezi zinazotolewa hapa nchini kama upandikizwaji wa viungo, tiba ya saratani, upasuaji wa moyo na kadhalika Mpango upo kwenye utaratibu wa kuanza kutoa huduma za ukusanyaji damu kwa kutumia mashine ya ‘’Apheresis’’.

Kwa kuboresha huduma Mpango wa Taifa wa Dama Salama chini ya Wizara ya Afya ulifanya manunuzi ya Mashine za Apheresis na kwa kuanza zimesimikwa katika kanda nne; Kanda ya Mashariki (Dar es salaam), Kanda ya Kusini Nyanda za Juu (Mbeya), Kanda ya Kaskazini (Moshi) na Kanda ya ziwa (Mwanza).

Mashine za Apheresis  ni maalumu ambapo mchangia damu hutoa mazao ya damu moja kwa moja  ambayo yana viwango na ubora wa kukidhi  matibabu maalumu na bobezi kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu.

Mpango wa Taifa wa Damu Salama, unaendesha mafunzo kwa wataalamu wa Mpango ili kuwajengea uwezo wa kuanza kutumia mashine hizo, mafunzo haya yanaendelea kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 27 hadi tarehe 30, 09-2022.