MAFUNZO YA UBORESHAJI HUDUMA ZA DAMU SALAMA

Posted on: March 27th, 2023

Mpango wa Taifa wa Damu Salama unaendelea kujenga uwezo katika vituo vyake vya Mikoa na Wilaya ili kuboresha huduma za Damu Salama Nchini, 

Tarehe 21-24/03/2023 Mpango umeendesha  mafunzo kwa kituo cha Damu Salama mkoa wa Manyara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha mazao ya damu na kuboresha huduma ya ukusanyaji damu kutoka kwa wachangia damu wa hiari, Mafunzo kama haya ni endelevu katika vituo vya mikoa yote Nchini.