MAFUNZO YA UWEZESHAJI HUDUMA ZA DAMU SALAMA MKOANI KIGOMA
Posted on: October 8th, 2023Mpango wa Taifa wa Damu Salama, unaendelea kujenga uwezo katika hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kuweza kutengeneza mazao ya damu na kuboresha ubora wa huduma za damu salama nchini. Tarehe 9.10.2023 hadi Tarehe 11.10.2023, Mpango unaendesha mafunzo kwa watumishi wa afya Mkoani Kigoma kwa kuwajengea uwezo wa kutengeneza mazao ya damu na matumizi sahihi ya damu. Akifungua mafunzo haya Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Stanley Binagi na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Mr. Nestory, wote wamesisitiza uwepo wa haki katika huduma za damu ni muhimu na kusisitiza kua damu haiuzwi.