MGANGA MKUU WA MKOA WA MOROGORO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA NA WARATIBU WA DAMU WA MIKOA

Posted on: August 29th, 2022

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kusirye Ukio Boniface, amefungua kikao kazi cha Mpango wa Taifa wa Damu Salama na waratibu wa Damu salama wa Mikoa, ambapo alitoa pongezi kwa hatua ya mafanikio ya Mpango, aidha alisisitiza umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa damu na mazao yake na kwamba damu inayokusanywa iwe yenye ubora unaokubalika kwa viwango vya kitaifa na kimataifa, alisisitiza pia malengo ya ya ukusanyaji wa damu yaendane na mahitaji yaliyopo katika vituo vya kutolea huduma.