Mpango wa Taifa wa Damu Salama watunukiwa Tuzo kutoka MSD

Posted on: March 6th, 2024

Mpango wa Taifa wa Damu Salama umetunukiwa tuzo kwa kuongoza mpango bila deni na cheti cha shukurani kwa ushirikiano mkubwa na MSD. Tunathamini sana heshima hii na tunajivunia kushirikiana na MSD katika kufanikisha malengo yetu ya afya katika taifa. Tunawashukuru kwa kuonesha imani na kuthamini mchango wetu. Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini. Asanteni sana kwa kutambua jitihada zetu.