MREJESHO WA UKAGUZI WA PROGRAM WA VIPIMO VYA UBORA WA MAKUNDI YA DAMU KUTOKA SANAS

Posted on: October 27th, 2024

Programu ya NBTS PT, inayohusika na uandaaji wa sampuli za kupima ubora katika eneo la utambuzi wa makundi ya damu, hivi karibuni imefanyiwa ukaguzi wa awali na wakaguzi kutoka Shirika la Afrika Kusini la Uidhinishaji wa Mifumo ya Kitaifa (SANAS). Ukaguzi huo ulifanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa programu hii inafuata miongozo ya ndani na ya kimataifa, ikiwemo viwango vya ISO 17043:2010, ambavyo ni vigezo muhimu kwa programu kupata ithibati ya kimataifa.

Katika ukaguzi huo, wakaguzi walichunguza kwa kina michakato na utaratibu wa programu ya NBTS PT na kutoa mrejesho kuhusu maeneo mbalimbali ya kuboresha ili kufikia viwango vinavyohitajika. Waliainisha maeneo muhimu yanayohitaji marekebisho ili kuhakikisha programu inakidhi viwango vya kimataifa vya ubora, usahihi, na kuaminika kwa huduma zinazotolewa.

Hatua hii ni muhimu kwa NBTS PT kwani itaiwezesha programu kupata ithibati inayotambulika kimataifa, hatua ambayo itaongeza ubora wa huduma za damu salama na kuimarisha sekta ya afya nchini.