WAZIRI WA AFYA MH: UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA

Posted on: April 10th, 2023

Waziri wa Afya. Mhe: Ummy Mwalimu ametembelea Makao makuu na kanda ya mashariki ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kuona hali ya upatikanaji wa damu na kufuatilia utekelezajaji wa maelekezo aliyoyatoa mwaka 2022 mwezi wa pili alipofanya ziara .

Aidha Mheshimiwa waziri ameridhishwa na utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa na pia amewashukuru Wananchi wanaoendelea kujitolea damu na amezitaka taasisi mbali mbali kushiriki katika kujitolea damu kama ambavyo club ya mpira ya yanga walifanya pamoja na taasisi za kidini kama wasabato (SDA) , Jai, Shia na wakatoliki.

Pia amegusia suala la wachangia damu wenye makundi adimu ambapo amepongeza wale waliojiunga na club na ameelekeza kuanza na watoto wanaozaliwa sasa hivi.. vile vile amewasisistiza wananchi kujua makundi yao ya damu ili kuweza kupata msaada wa haraka wanapohitaji damu.